Jumanne 10 Juni 2025 - 21:51
Vyama vya siasa vya Ufaransa vyaendelea kutaka kuachiliwa kwa waendesha kampeni wa Meli ya Madeleine

Hawza/ Wajumbe wa mrengo wa kushoto katika Bunge la Ufaransa katika taarifa yao wamesema: Kukamatwa kwa waendesha kampeni za haki za binadamu katika meli ya misaada kuelekea watu wa Ghaza ni uvunjaji wa wazi wa haki za kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza,  wajumbe wa mrengo wa kushoto katika Bunge la Ufaransa katika taarifa yao wamesema: Kukamatwa kwa waendesha kampeni ya haki za binadamu katika meli ya misaada kuelekea watu wa Gaza ni uvunjaji wa wazi wa haki za kimataifa.

Meli ya Uingereza iitwayo Madeleine ilianza safari kwa lengo la kuvunja kizuizi kigumu kilichowekwa na utawala wa Israel dhidi ya watu maskini wa Ghaza. Utawala unaomwaga damu wa Kizayuni umewaua karibu watu 55,000 tangia Oktoba 2023 katika mashambulizi yake ya kutisha.

Vitu vilivyokuwepo kwenye meli hiyo vilijumuisha; maziwa ya unga na vyakula kwa ajili ya watoto, ambavyo vilikamatwa na vikapigwa marufuku usiku mmoja kabla ya meli hiyo kufika katika pwani ya Ukanda wa Ghaza na vikapelekwa baadaye katika bandari ya Ashdod huko Israel na vikawa chini ya usimamizi wa majeshi ya Israel.

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa kuikamata meli hiyo peke yake ni uvunjaji wa sheria za kimataifa, na hata zaidi ya hayo, kumkamata kabisa ni jambo la kutisha. Wao pia waliitaka jamii ya kimataifa kuitaka vikali jinai hii kubwa na pia wakaomba utawala wa Israel kuwaachilia huru mara moja na bila masharti yoyote waendesha kampeni wa haki za binadamu waliokuwepo kwenye meli hiyo.

Chama cha kijani cha Ufaransa pia kililaani jinai hiyo ya Israel na kusisitiza kuwa, kukamatwa kwa waendesha kampeni za haki za binadamu yanapaswa kupingwa kwa kiwango cha dunia nzima, jambo ambalo linaanza na Serikali ya Ufaransa na linapaswa kuendelea hadi Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa na kuwa jambo la pamoja.

Kwa jumla, watu 12 walihudhuria kwenye meli hiyo kama waendesha kampeni ya haki za binadamu, wakiwemo 11 kutoka nchi za Sweden, Ufaransa, Hispania na Ujerumani, pamoja na mwandishi mmoja wa habari.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha